Add parallel Print Page Options

Tazama, Yesu anakuja pamoja na mawingu! Kila mtu atamwona, hata wale waliomchoma.[a] Watu wote wa dunia watamwombolezea.[b] Ndiyo, hili litatokea! Amina.

Bwana Mungu asema, “Mimi ni Alfa na Omega.[c] Mimi ndiye niliyepo, aliyekuwepo na anayekuja. Mimi ni Mwenye Uwezo Wote.” Mimi ni Yohana, mwamini mwenzenu. Tuko pamoja katika Yesu na tunashirikiana mambo haya: mateso, ufalme na uvumilivu wenye subira. Nilikuwa katika kisiwa cha Patmo[d] kwa sababu nimekuwa mwaminifu kwa ujumbe wa Mungu na kwa ajili ya kweli ya Yesu.

Read full chapter

Footnotes

  1. 1:7 waliomchoma Yesu alipouawa, alichomwa mkuki ubavuni. Tazama Yh 19:34.
  2. 1:7 watamwombolezea Ama, “watajipiga vifuani mwao”. Usemi huu unatumika kuonesha huzuni na majonzi kwa yaliyomtokea pia hii ni ishara ya kuomboleza. Neno la Kiyunani lina maana ya kitendo zaidi ya kilio kwa sauti.
  3. 1:8 Alfa na Omega Herufi ya kwanza na ya mwishi katika mfumo wa herufi wa Kiyunani, hapa inamaanisha “wa Kwanza na wa Mwisho”.
  4. 1:9 Patmo Kisiwa kidogo katika bahari ya Aegeani. Kisiwa hiki kiko karibu na pwani ya nchi ya Uturuki kama inavyojulikana siku za leo.